Genesis 30:22-27

22 aNdipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. 23 bAkapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

24 cAkamwita Yosefu
Yosefu maana yake Yeye na aongeze, yaani Mungu na aniongezee.
na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.”

Makundi Ya Yakobo Yaongezeka

25 eBaada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu. 26Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.”

27 fLakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba Bwana amenibariki kwa sababu yako.”
Copyright information for SwhNEN